Prof, Daktari, Tigiti Shaaban Yusuf SengoProf. Emmanuel Mbogo2025-08-122025-08-12https://dspace.academy.edu.ly/handle/123456789/1705Vilevile, Kiswahili kikawa ndiyo lugha ya mawasiliano katika shughuli zote za utawala serikalini ambapo mikutano, mijadala na huduma kwa wateja vilifanywa kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Shughuli za mahakama nazo zilifanywa kwa kutumia lugha ya Kiswahili sambamba na Kiingereza hasa katika mahakama kuu. Hatua ya kukitangaza Kiswahili kuwa lugha ya taifa si tu kwamba lilikuza matumizi ya lugha ya Kiswahili bali pia lilisaidia sana katika kuwaunganisha Watanganyika na kuwafanya kuwa kitu kimoja (Mekacha, 2000).Kiswahili imekuwa na inaendelea kuwa lugha muhimu sana katika maendeleo ya bara la Afrika na duniani kwa jumla (Mulokozi, 2002). Umuhimu huo unaonekana pale ambapo lugha ya Kiswahili imekuwa ni chombo cha kuwaunganisha watu wa jamii na utamaduni tofauti kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Pia Kiswahili kimekuwa ni lugha ya biashara na mawasiliano ya kimataifa (Ghanem, 2005; Dzahane, 2013).SHAHADA ZA JUU ZA KISWAHILIKUCHUNGUZA MAFANIKIO NA CHANGAMOTO ZA WAHITIMU WA KILIBYA WA SHAHADA ZA JUU ZA KISWAHILI